MAJAMBAZI YA KIKE YANASWA NA SILAHA NANE ZA KIVITA, FUKWE ZA BAHARI
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es
Salaam limekamata watuhumiwa 10 wa
ujambazi, wakiwamo wanawake wawili
waliokutwa na silaha nane za kivita
kufuatia msako uliofanywa na jeshi hilo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya
Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema
majambazi hao walikuwa katika mtandao
wa ujambazi wa kufanya uhalifu katika
maeneo tofauti.
Alisema polisi wameimarisha ulinzi katika
maeneo yote, ikiwamo katika nyumba za
ibada kwa ajili ya Sikukuu ya Iddi El-Fitri
kwa kushirikiana na vyombo vingine,
vikiwamo Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji
pamoja na kampuni binafsi za ulinzi.
“Tumejipanga kuimarisha ulinzi
kutumia kikosi cha Kutuliza Ghasia
(FFU), kwa kutumia magari
maalumu, mbwa, farasi
waliofundishwa ulinzi na usalama,
kikosi cha wanamaji na wale wa
usalama barabarani,” alisema
Kamanda Kova.
Alisema polisi watatoa ulinzi katika fukwe
za bahari kwa kuweka vituo vya polisi vya
muda katika maeneo hayo ili kuhamasisha
ulinzi ili kutoa msaada wa haraka
utakapohitajika.
“Tunawaomba wazazi walezi kuwa
makini na watoto, ambao
wanahitaji kuangaliwa usalama
wao katika fukwe za bahari na
maeneo ya kuogelea, licha ya Jeshi
la Polisi kuwapo katika baaadhi ya
fukwe za bahari kuangalia ulinzi
na usalama,” alisema Kamanda
Kova.
Chapisha Maoni