0
Ndege ya AirAsia



Shirika la ndege la AirAsia linasema kuwa limeanzisha shughuli ya kuitafuta ndege yake iliyopoteza mawasiliano na kituo cha kuelekeza safari za ndege dakika 45 baada ya kuondoka
kwenye mji wa Surabaya nchini Indonesia.

Zadi ya watu 160 walikuwa ndani ya ndege hiyo ya Airbus 320 iliyokuwa safarini kwenda nchini Singapore.

Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanatoka nchini Indonesia.

Msemaji wa wizara ya usafiri nchini Indonesia amesema mawasiliano yalipotea kati ya visiwa vya
Kalimantan na Java. Wataalamu wa safari za ndege wanasema kuwa huenda ndege hiyo iliishiwa na mafuta

Chapisha Maoni

 
Top