0
BEKI John Terry atasaini Mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Chelsea baada ya kocha Mreno, Jose Mourinho kusema mpango huo unaandaliwa.

Beki huyo wa kati mwenye umri wa miaka 34 ataongoza mbio za kuwania tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwa wa Kulipwa (PFA) kutokana na kufanya kwake vizuri hivi sasa akicheza katika
safu ya ulinzi.Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amesema jana kwamba Terry bado mchezaji muhimu kwake. "Hakuna shaka atapewa Mkataba mwingine. 

Nafahamu hilo, anafahamu pia. Tupo
katika klabu, katika bodi tunafahamu hilo na pia unatakiwa kufikiria hilo,".
"Bila sisi kuthibitisha hilo, unatakiwa ufikirie hivyo. Ni mchezaji muhimu sana katika timu, hivyo mkataba mpya unakuja haraka iwezekanavyo. Ni utaratibu tu," amesema.

Chapisha Maoni

 
Top