MASTAA nane wa klabu ya Msimbazi
wamekacha timu hiyo iliyoandoka leo
kwenda Zanzibar kwa kile wanachoshinikiza kulipwa fedha zao.
Habari za kuaminika zinasema kuwa
mastaa nane wa klabu hiyo wameingia
mitini wakiwemo waganda watano na
wabongo watatu mpaka hapo
watakapomaliziwa fedha zao za usajili.
Wabongo waliokacha timu hiyo ni Shaban Kisiga, Jonas Mkude na Ivo Mapunda hata hivyo kocha msaidizi wa timu hiyo Seleman Matola jana alikiri kutokuwepo kwenye kikosi chake wachezaji hao na kuweka wazi kuwa Ivo amekwenda Mbeya kwenye arobaini ya mama yake mzazi aliyefariki hivi karibuni, huku akiwa hana taarifa za
wachezaji waganda ambao wameingia
mitini ni Emmanuel Okwi ambaye alikuwa wa kwanza kutimka mara baada ya kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Kagara.
Wengine ni Joseph Owino, Dan Sserunkuma, Juuko Murshid na Simon Sserunkuma.
"Ninaondoka na wachezaji wachache, nina taarifa za Ivo tu ambaye ameenda kwenye harobaini ya mama yake, wengine sina taarifa zao." alisema Matola ambaye hata hivyo ameaidi kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri kwenye michuano ya Kombe
la Mapinduzi.
Kikosi hicho cha Simba kimeondoka leo
asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa
michuano ya Kombe la Mapinduzi
itakayoanza kutimua vumbi keshoJanuari Mosi hadi Januari 13 kwenye uwanja wa Aman visiwani Zanzibar.
Mwenyekiti wa kamati ya usajili Zakaria
Hanspope alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema kwa kifupi "Nipo Iringa, sijui chochote kinachoendelea Simba kwa sasa, hayo mambo waulizeni viongozi waliopo huko, mi mwenyewe nasikia tu lakini sijui
chochote."
Mwenyekiti wa Simba Evans Aveva
hakupatikana kuzungumzia suala hilo, hata hivyo mmoja wa viongozi wa klabu hiyo aliiambia Mwananchi kuwa wachezaji hao waliondoka kwa vile Simba hawakuwa na uhakika wa kushiriki michuano ya Kombe la
Mapinduzi.
"Unajua barua ya kuthibitisha yenyewe
imetumwa juzi tu, hatukuwa na uhakika wa kushiriki ndio maana tuliwaruhusu
wachezaji kuondoka na warudi tarehe
moja, wote wana ruhusa maalum."alisema mmoja wa viongozi wa wekundu hao wa Msimbazi.
Chapisha Maoni