Mahakama moja ya Misri imepunguza hukumu ya watu wanane waliodaiwa kushiriki katika ndoa ya watu wa jinsia moja kutoka miaka mitatu hadi
mwaka mmoja.
Mwezi Uliopita ,wanane hao walipatikana na hatia ya kuchochea uasherati.
Walishtakiwa baada ya kanda moja ya video kusambaa katika mitandao ikiwaonyesha wakisherehekea katika boti moja lililokuwa mto
Nile huku wanaume wawili wakionekana
wakivalishana pete na kukumbatiana.
Watu hao baadaye walikataa kwamba ilikuwa harusi ya watu wa jinsia moja.
Ushoga ni kinyume na utamaduni wa
Misri ,ijapokuwa si kinyume na sheria.
Wanaharakati wa kupigania haki za kibinaadamu wanasema kuwa kampeni dhidi ya mashoga imeimarishwa katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni nchini Misri.
Africa Newss
Chapisha Maoni