Siku kadhaa baada ya kuanza kwa kambi ya
mazoezi kwa ajili ya matayarisho ya msimu mpya
wa ligi nchini Tanzania, tayari imethibitishwa kuwa
kikosi cha Mbeya City fc kitasafiri mpaka mkoani
Morogoro kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu
dhidi ya wenyeji Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa
Jamhuri julai 30.
Kwa mujibu wa kiongozi wa Kanisa la Faith
Baptist, Mch Jerry Wyatt ambaye ndiye mwandaaji
na msimamizi mkuu wa mchezo huo,amesema
maandalizi yote ya mechi hiyo ya kirafiki
itakayoambatana na tamasha kubwa la mahubiri ya
neno la Mungu tayari yamekamilika ikiwa ni
pamoja na timu zote kuthibitisha kuhudhuria.
Maandalizi yote yamekamilika, timu zote
zimethibitisha kushiriki katika mchezo huo ambao
utaambana na mahubiri ya neno la Mungu kwenye
uwanja wa Jamhuri, naomba watu wajitokeze kwa
wingi kuja kushuhudia mchezo mzuri wa kirafiki
kutoka kwa timu hizi mbili pia kupata mahubiri
mazuri ya neno la Mungu hakutakuwa na kiingilio
chochote kwa watakaofika kwenye uwanja wa
Jamhuri .
Hii ni mara ya pili kwa Mtibwa na City kucheza
mchezo wa kirafiki ulioandaliwa na Kanisa hilo
awali ikiwa ni msimu uliopia ambapo timu hiyo
kutoka Manungu iliibuka na ushindai wa bao 1-0
lililofungwa kipindi cha pili na Mohamed Ibrahim
City inatarajia kuondoka Mbeya Julai 28 tayari kwa
mchezo huo uliopangwa kupigwa siku jumamosi
ya mwisho wa mwezi huo
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni