0
“Unapotwaa ubingwa inakupa nafasi
kubwa katika mbio za kuwania tuzo ya
Ballon d’Or, mwaka huu Ronaldo
ameshatwaa ubingwa wa Ligi ya
Mabingwa na sasa ana wa Euro 2016,
hivyo naweza kusema yupo kwenye
nafasi nzuri,” alisema nyota nyota straika
wa Barcelona, Neymar.
Kwa maneno haya ni kama amempa tuzo
ya mchezaji bora wa dunia FIFA Ballon
d’Or, nyota wa Real Madrid, Cristiano
Ronaldo baada ya kusema kwamba yuko
njiani kutwaa tuzo hiyo.
Ronaldo aliiwezesha Real Madrid kutwaa
ubingwa wa Ligi ya Mabingwa msimu wa
2015/16 baada ya kuifunga Atletico
Madrid kwa bao 1 kwa nunge na kisha
akaiwezesha timu ya taifa ya Ureno
kuondoka na ushindi wa fainali za Euro
2016 dhidi ya waliokuwa wenyeji,
Ufaransa.
Kwenye utetezi wa tuzo za msimu
uliopita, nyota huyo alishika nafasi ya pili
nyuma ya mpinzani wake, Lionel Messi,
lakini kwa sasa Neymar anasema
kwamba anavyoamini kinara huyo
mwenye umri wa miaka 31 safari hii
yupo kwenye nafasi ya kutwaa tena tuzo
hiyo.
Pia, mbali na hilo Ronaldo ni mchezaji
mahiri na inasemekana kwamba katika
hilo hana wasiwasi nalo.

Chapisha Maoni

 
Top