Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini wanasema
watakata rufaa kwa mara nyingine tena kupinga
hukumu wanayoielezea kama hafifu mno alipopewa
Oscar Pistorius ya miaka sita pekee jela kwa kosa
la kumuua mpenzi wake mwaka 2013.
Bingwa huyo wa zamani wa mbio za Olimpiki za
walemavu, Pistorius mwenye umri wa miaka 29,
alihukumiwa miaka 6 jela na jaji Thokozile Masipa
baada ya kupatikana na kosa hilo la kuumua Reeva
Steenkamp siku ya wapendanao 2013.
Katika rufaa ya awali, alikuwa amekabiliwa na
uwezekano wa kufungwa jela zaidi ya miaka 15.
Uamuzi huo ulikuwa umetolewa baada ya
kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya kuua bila
kukusudia wakati jaji huyohuyo Thokozile Masipa
alimpa kifungo cha miaka mitano tu jela akisema
Pistorius hakukusudia kuua na alidhania
amevamiwa na mwizi ndio akafyatua risasi bila
kujua ni Reeva Steenkamp aliyekuwa nyuma ya
mlango wa bafu.
Oscar Pistorius afungwa jela miaka sita
Hoja hiyo inalopingwa vikali na kambi ya
mwendesha mashtaka wakisema Pistorius alijua
bayana aliyekuwa akimfatulia risasi ni Reeva kwani
walikuwa wote nyumbani kwake siku hiyo ya
Valentine, na huenda wapenzi hao walikuwa na
ugomvi baina yao .
Upande wa utetezi ulikuwa umesema hawangekata
rufaa kwa hukumu hiyo ya pili ya miaka sita.
Upande wa mwendesha mashtaka unasema iwapo
hawatapigania haki, kwamba Pistorius apewe
kifungo kirefu inavyostahili kwa makosa hayo ya
mauaji, basi itakuwa mfano mbaya utakaofanya
mfumo wa sheria Afrika Kusini udharauliwe.
Wazazi wake Reeva wamesema wanaunga mkono
juhudi zote zinazofanywa na waendesha mashtaka
kupata haki, na kwamba kifo cha wanawao
kimewaathiri vibaya sana kiasi cha kuwasababishia
maradhi.
Wanapanga kufungua wakfu kwa jina la mwana
wao Reeva aliyekuwa anajulikana sana kama
mwanamitindo mwenye sura ya kupendeza.
Posted Africa News Sports
Chapisha Maoni