0
MREMBO wa Tanzania wa mwaka 2013,
Happiness Watimanywa ameahidi
kuing’arisha Tanzania katika mashindano ya ulimbwende ya Dunia yatakayofanyika mapema mwezi ujao huko nchini Uingereza.

Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, mlimbwende huyo
amewaeleza waadishi kuwa, kutokana na uzoefu wa kazi zake alizokuwa akifanya kwa jamii kwa muda kipindi cha mwaka
mmoja ikiwemo misaada ya hali na mali
anayoipata toka Bodi ya Utalii Tanzania
pamoja na wahisani wengine nchini
amewaahidi Watanzania kuibuka na
ushindi katika kinyang’anyiro hicho huko
nchini Uingereza ili kuitangaza Tanzania.
Alieleza kuwa, tayari Ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza utakuwa tayari kumpokea pindi atakapowasili nchini humo kwa lengo la kuiwakilisha Tanzania katika
mashindano hayo ya ulimbwende
yatakayowahusisha walimbwende toka
Ulimwengu mzima.
“Nimejifunza mambo mengi hasa kipindi
wakati nasafiri sehemu mbalimbali nchini pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii katika kipindi chote, hivyo nawaahidi
watanzania ushindi katika mashindano
hayo yatakayofanyika huko Uingereza pia mnipigie kura zenu za wingi”, alisema Watimanywa.
Naye Mkurugenzi wa Lino International
Agency Limited, Bw. Hashim Lundenga
ambao ni waandaaji wa Miss Tanzania,
alisema kuwa mashindano ya Urembo wa
Dunia ni mashindano ya Kimataifa ambayo yanawakutanisha walimbwende toka nchi nyingi duniani ikiwemo Tanzania, hivyo alitoa wito kwa watanzania wote kuunga mkono kwa kumpigia kura nyingi mwakilishi ambaye ndiye mrembo wa Tanzania kwa mwaka 2013, Hapinness Watimanywa ili ajinyakulie taji hilo la dunia ili aweze kuipa sifa Tanzania kimataifa.

Mashindano ya Urembo ya Dunia
yanatarajiwa kufanyika mapema tarehe 14 Desemba, 2014 huko nchini Uingereza ambapo mrembo huyo wa Tanzania anatarajia kuanza safari yake ya kuelekea nchini humo tarehe 15 Novemba, 2014 tayari
kwa ajili ya mashindano hayo.

Chapisha Maoni

 
Top