0
Baadhi ya Wabunge wameomba mwongozo wa kutaka kuchunguzwa kwa Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Bwana Willison Kabwe kutokana
tuhuma za kuipatia kazi kampuni ya Tanzania Buildings Works ambayo imeshindwa kutekeleza miradi ya ujenzi katika mikoa yote aliyoiongoza
ikiwemo Mbeya na Mwanza na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni Tatu.

Akiomba mwongozo wa spika kufuatia kauli ya waziri wa ujenzi Dkt John Magufuli wa kutaka kuchunguzwa kwa kampuni hiyo, Mbunge wa Rombo Mhe. Joseph Selasini alisema mkurugenzi
huyo chini ya uongozi wake ndio ametoa kazi kwa kampuni hiyo ambayo alipohamishiwa mkoani Mwanza pia aliipa kazi na kusababisha hasara
kubwa.

Akitoa mwongozo, mwenyekiti wa kikao Mhe. Mussa Azzan Zungu aliitupia lawama serikali kwa kutosikiliza malalamiko ya wananchi na kuwahamisha viongozi wabovu wanaotenda makosa toka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine.

Chapisha Maoni

 
Top