Moreno Ocampo alyekuwa kiongozi wamashtaka wa ICC na kiongozi wa sasa wa mahakama hiyo Fatou bensouda
Mwendesha mashtaka mkuu kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita Fatou Bensouda
amesema kuwa atasitisha uchunguzi kuhusu uhalifu wa kivita ulioendeshwa katika eneo la Darfur nchini Sudan kutokana na ukosefu wa
usaidizi kutoka kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa.
Kwenye taarifa yake kwa baraza hilo mwendesha mashtaka huyo amesema kuwa wanawake na wasichana wanaendelea kuathirika zaidi katika
jimbo hilo.
Rais wa Sudan Omar El Bashir anayetafutwa na mahakama ya ICC kwa kuhusishwa na uhalifu dhidi ya binaadamu katika eneo la DarfurAmesema kuwa kutokuwepo kwa hatua zozote kutoka kwa baraza la umoja wa mataifa kumechangia kuendelea kwa uhalifu na sasa amelazimika kutumia raslimali za mahakama hiyo
kwa masuala mengine.
Mwaka 2009 mahakama ya ICC ilimhusisha rais wa Sudan Omar al-Bashir na uhalifu wa kivita kwenye
jimbo la Darfur lakini hadi sasa hajakamatwa wala hata mmoja wa washirika wake.
Chapisha Maoni