0

Mastaa wa Tanzania Nasibu Abdul a.k.a Diamond Platnumz na Omary Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz, nyimbo zao zimetajwa kuwania tuzo za
HiPipo Music Awards (HMA2015) za Uganda zinazotarajiwa kutolewa mwakani.

‘Number One’ (original) ya Diamond na
‘Ndagushima’ ya Dimpoz zinachuana na nyimbo zingine za Afrika Mashariki kwenye kipengele kimoja cha East Africa Super Hit.

Nyimbo za Ommy na Diamond zitakuwa
zikichuana na ‘Nishike’ ya Sauti Sol na ‘Kioo’ ya Jaguar. Nyimbo nyinginne kwenye kipengele hicho
ni Baramushaka – Knowless, Sitya Loss – Eddy Kenzo, Tayali – Urban Boys Ft Iyanya pamoja na Love You Everyday – Bebe Cool.

Tuzo za HiPipo Music Awards 2015 (HMA2015) zitatolewa siku ya Jumamosi Feb.7, 2015


Chanzo: HiPipo

Chapisha Maoni

 
Top