0
REAL Madrid wameangukia pua Uwanja wa Mestalla, baada ya kufungwa mabao 2-1 na wenyeji Valencia katika mchezo wa la Liga usiku huu.

Kipigo hicho kinaamanisha wimbi la ushindi la Real Madrid katika mechi 22 mfululizo limezimwa na Valencia. Cristiano Ronaldo alitangulia kuifungia Real kwa penalti dakika ya 14 tu ya mchezo huo, baada ya Alvaro Negredo
kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.

Beki wa Valencia, Antonio Barragan Fernandez akaisawazishia timu yake dakika ya 52, kabla ya Nicolas Otamendi kufunga la ushindi dakika ya 65 kwa kichwa akimalizia kona ya Daniel
Parejo.

Kikosi cha Valencia kilikuwa; Diego Alves, Barragan/Feghouli dk73, Otamendi, Mustafi, Orban, Parejo, Enzo Perez, Andre Gomes, Piatti/
Gaya dk23, Negredo/Rodrigo dk80 na Alcacer.

Real Madrid: Casillas, Carvajal, Ramos, Pepe, Marcelo, Isco, Kroos, James/Khedira dk71, Bale/Jese dk71, Benzema/Hernandez dk80 na
Ronaldo.

Chapisha Maoni

 
Top