Klabu ya Barcelona imetangaza ipo tayari kumuachia beki wake, Jeremy Mathieu katika usajili wa kiangazi licha ya kuwa mlinzi huyo wa kati amebakiza mkataba wa mwaka mmoja kikosini hapo.
Mathieu alikuwa akikabiliwa na majeraha mwaka jana na ataondoka klabuni hapo kwenda klabu yoyote itakayofikia dau la Pauni 2.4 milioni.
Hata hivyo, Barcelona na mchezaji huyo walikubaliana kuendelea kumlipa licha ya kukuwapo uwanjani. Mchezaji huyo miaka 33 ameitumikia klabu hiyo kwa takribani miaka minne sasa akiwa amecheza mechi 86 na kufunga mabao sita.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.