0
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini 'TFF' limethibitisha kupokea barua ya zuio la kuendelea na mchakatto wa uchuguzi kutoka Baraza la Michezo la Taifa 'BMT', Lakini wamesisitiza kwamba uchaguzi huo utaendelea kama ulivyopangwa.
Akizungumza na Vyombo vya habari Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema walichelewa klupokea barua hiyo lakini kwa kuwa tayari imefika kwenye ofisi zao basi wataifanyia kazi mara moja huku mchakao wa uchaguzi ukiendelea.
-Tumeipokea Barua ya BMT, tumeitisha kikao cha TFF na tutaijadili na kuifanyia kazi, lakini mchakato wa uchaguzi utaendelea kama ilivyopangwa" Alisema Alfred.
Ikumbukwe kwamba Jumanne ya Juni Juni 13 Baraza la michezo la Taifa BMT Kupitia kwa katibu Mkuu Mohamed Kiganja liliagiza kusimamishwa kwa uchaguzi wa TFF ambao umepangwa kufanyika Agosti 12, hadi pale watakapofuata utaratibu wa kullitaarifu Baraza hilo.
Taratibu za Uchaguzi.
Wakati hayo yakiendelea TFF wameendelea kusisitiza na kuwaalika wanafamilia wote wenye nia ya kuwania uongozi katika shirikisho hilo kujitokeza kuchukua fomu kuanzia Juni 16, mwaka huu.
PIA SOMA: TFF Yapuliza Kipyenga cha Kumpata mrithi wa Jamal Malinzi.
Huku wakidai kwamba Tarehe ni ileile iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Revocatus Kuuli alipozungumza na wanahabari Jumatatu wiki alipotangaza ratiba nzima ya Uchaguzi Mkuu wa TFF uliopangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
TFF imeendelea kusema kuwa Kwa kuwa tovuti yao kwa sasa ipo kwenye marekebisho, hivyo zoezi la kuchukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi TFF zitatolewa kwenye ofisi za TFF zilizopo Ilala, Dar es Salaam kuanzia asubuhi ya Juni 16, 2017 hadi saa 10 jioni siku ya Juni 20, mwaka huu.
Fedha za kulipia fomu hizo zitalipiwa Benki ya CRDB kupitia namba ya akaunti 01J1019956700 ambako mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka benki na kupewa fomu ya nafasi husika.
Gharama za kuchukulia fomu ni.
1. Rais TSHS 500,000/=
2. Makamu wa Rais TSHS 300,000/=
3. Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/=

Chapisha Maoni

 
Top