0
Kikosi cha wachezaji 20 wa Timu ya Soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na Benchi la Ufundi lenye watu 7 na Viongozi wawili wamewasili Salama Mjini Kigali, Rwanda.
Msafara huo ambao uliondoka Asubuhi ya Jumatano Jijini Mwanza kuelekea Dar es Salaam ambapo waliunganisha Ndege ya kuelekea Rwanda, wamewasili Salama na Tayari wameanza kujifua kuelekea mchezo wa Marudiano dhidi ya wenyeji Rwanda Jumamosi ya Julai 22.
Mkuu wa msafara Alhaj Ahmed ' Msafiri ' Mgoyi, ameuthibitishia mtandao huu kuwa kikosi kipo katika Hali nzuri na kwamba lengo lao ni kuona wanaibuka na ushindi ili kuweza kusonga mbele.
-Kikosi kimewasili Salama na asubuhi tumeanza mazoezi, ukiangalia matokeo ya mchezo wa awali inatulazimu mchezo huu tuweze kushinda au Sare ya Mabao Mengi, tunamuona Mwalimu anahangaika na hilo na tunaamini dhamira yetu Itatumia' Mgoyi Alieleza.
Mchezo wa Awali.
Tanzania watashuka Dimbani Jumamosi ya Julai 22 kucheza na Rwanda katika mchezo wa Marudiano wa kuwania Kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za Ndani Yaani 'CHAN'.
Katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza Timu hizo Zilitoka Sare ya Bao 1-1 na hivyo ili Tanzania waweze kuingia raundi nyingine wanapaswa kuibuka na ushindi wa Aina yoyote au Sare ya kuanzia Mabao mawili.
Hata hivyo kama Tanzania Wanafuzu watakutana na Mshindi wa mchezo kati ya Uganda na Sudan Kusini katika raundi ya mwisho ya mchujo kuwania Kufuzu katika mashindano hayo yatakayofanyika mwakani nchini Kenya.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top