Kijana Aukata Ulimi Wake Na Kuutoa SADAKA Kwa Mungu
KIJANA
Lalmohan
Soren
(17)
amekata
sehemu
ya
ulimi
wake
kwa
wembe
kutokana
na
imani
kali
ya
dini
kwa Mungu wake wa Kihindu. Soren
aligundulika kukata sehemu ya ulimi
wake nyakati za asubuhi alipokaa ndani
ya msikiti wa Mahedevgarha katika eneo
la Dugda, Jharkhand ndipo waumini
walipoona damu imetapakaa sakafuni.
Waumini hao waliacha kusali na
kuangalia zaidi ndipo wakakuta ulimi huo
upo ndani ya bakuli pembeni ya Soren
aliyekuwa hawezi kuzungumza.
Sambamba na bakuli hilo waliona karatasi
iliyoandikwa “nimeukata ulimi wangu na
kuutoa kama sadaka kwa Mungu Shiva”.
“Tafadhali msiniondoe hapa msikitini,
nataka nikae hapa miguuni kwa Mungu”.
Soren alitoa sadaka ulimi wake kwa
Mungu Shiva kwa lengo la kumfurahisha
na pia kutimiza ndoto zake. Kutokana na
tukio hilo, kiongozi wa msikiti huo
alitaarifiwa na akafanikiwa kumshawishi
Soren akubali kupelekwa hospitali.
Madaktari walijaribu kuushona ulimi huo
kwa lengo la kuurejesha sehemu
ulipokuwepo awali, lakini walishindwa na
baada ya siku chache Soren aliruhusiwa
kutoka hospitalini. Kwa sasa Soren yupo nyumbani na
anaendelea kupona, lakini hawezi tena
kuzungumza na amekuwa akipewa
chakula cha majimaji. Hata hivyo, Soren
mwenyewe hajutii kitendo alichokifanya
na amekuwa akijivunia kwa ujasiri na
kumfurahisha Mungu Shiva.
Kutokana na kitendo hicho, familia yake
imeshtushwa, lakini imekubaliana na hali
hiyo. Mama wa Soren anasema “mwanagu
amekuwa akijihusisha na mambo ya dini
tangu akiwa mtoto”. “Amekuwa akipenda dini sana, lakini
sikuamini kama ipo siku atakata ulimi
wake kumfurahisha mungu. Sijui
kitakachotokea kwake lakini najua
hataweza tena kuzungumza vizuri. Maisha
yake ya baadaye yatamtegemea Mungu
zaidi”. Hata hivyo, mama huyo mwenye
watoto wanne, ana uhakika Soren atapata
baraka.
“Mwanangu amejitolea ulimi wake
kumfurahisha mungu hivyo tuna hakika
mungu atatimiza maombi yake yote na
kumpa maisha mazuri”, anasema mama
huyo. Watu wa eneo hilo wameshangazwa
na jinsi vyombo vya habari
vilivyolichukulia suala hilo kwani wao
wanaona ni kitu cha kawaida kutokea.
Jirani wa Soren, Manoj Sharma anasema;
“watu wa eneo hili ni washirikina sana na
siku zote wanatekeleza mambo ya ajabu.
Mwaka 2011 kijana mmoja alijikata vidole
viwili na kutoa sadaka kwa Mungu katika
msikiti huohuo, hivyo tukio hili si jipya
ingawa linaumiza nafsi za wengi.”
Chapisha Maoni