Msanii wa Nigeria anaetamba na hits kibao, Davido ataingia Tanzania mwishoni mwa mwezi huu na kufanya show kubwa November 1.
Msanii huyo analetwa na kituo cha radio cha 100.5 Times Fm kupitia tamasha lake jipya lililopewa jina la ‘The Climax’.
Tayari vidokezo vya show hiyo vimeanza
kurushwa kwenye kituo hicho cha radio huku orodha ya mengi yatakayofanyika ikitarajiwa kuwekwa wazi muda wowote kuanzia leo.
Davido ambaye ni mshindi wa tuzo kadhaa kubwa ikiwemo tuzo ya BET na MTV (MAMA) anatamba na hits kadhaa ikiwemo Skelewu, Aye, tchelete na
nyingine nyingi.
Kaa mkao wa kushangweka na kilele cha burudani cha mwaka ‘The Climax’ ya 100.5 Times FM. “Paris was Great next stop!! LONDON –LAGOS-
WARRI-SOUTH AFRICA-NAMIBIA-TANZANIA lego.”
Ameandika Davido kwenye Instagram.
Chapisha Maoni