IKIONGOZWA na kiungo mahiri Mkenya, Victor Wanyama, Southampton imefanikiwa kuvuna pointi moja ugenini baada ya sare ya 1-1 na wenyeji Aston Villa usiku wa jana Uwanja wa
Villa Park.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya England, Gabriel Agbonlahor aliwafungia wenyeji bao la kuongoza dakika ya 29 akitumia vizuri makosa ya kipa Fraser Forster.
Nathaniel Clyne aliisawazishia Southampton zikiwa zimebaki dakika tisa mchezo kumalizika na sare hiyo inafanya wageni hao wabaki wanazidiwa pointi sita na vinara wa Ligi Kuu, Chelsea, wakati Villa wanapandaa juu ya Hull nafasi ya 16.Watu 25,311 tu walihudhuria mechi hiyo- hayo yakiwa mahudhurio mabovu zaidi tangu walipomenyana na Sheffield Wednesday Desemba 1999 walipocheza mbele ya watu 23,885.
Kikosi cha Aston Villa kilikuwa; Guzan, Hutton, Okore, Clark, Cissokho, Westwood, Sanchez/ Bent dk74, Weimann, N’Zogbia/Richardson
dk64, Cleverley na Agbonlahor.
Southampton; Forster, Clyne, Fonte,
Alderwiereld, Bertrand, Wanyama, Schneiderlin, Tadic, Long/Cork dk89, Mane/Mayuka dk79 na
Pelle.
Chapisha Maoni