Licha ya watu mbalimbali kutaka Rais Jakaya Kikwete kumwajibisha Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kuhusiana na sakata la fedha za escrow, Ikulu imesema suala hilo litatolewa uamuzi wakati wowote
baada ya mapumziko ya sikukuu.
Hivi sasa Rais yupo katika mapumziko ya Sikukuu za Krismasi inayosherehekewa Desemba 25 kila mwaka na Mwaka Mpya itakayofanyika Januari Mosi.
Akizungumza na wazee wa Dar es Salaam Desemba 22 mwaka huu, Rais Kikwete alisema amemweka kiporo waziri huyo hadi atakapopata ufafanuzi wa mambo kadhaa na kwamba atakapojilidhisha ataujulisha umma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue aliliambia gazeti hili jana kuwa Rais Kikwete bado hajakamilisha kulishughulikia suala hilo na kwamba litakapokuwa tayari wananchi
watajulishwa hatua alizozichukua.
“Unakumbuka Rais alichosema? Bado
analifanyia kazi, atakapomaliza tu mtajulishwa, sasa hivi ni kipindi cha sikukuu,” alisema Sefue.
Profesa Muhongo
Hata hivyo, Profesa Muhongo alipotakiwa kuzungumzia shinikizo linalotolewa la kutaka ajiuzulu kabla ya Rais Kikwete kutoa uamuzi wake, aliliambia gazeti hili jana kwa simu
kuwa; “Mimi sasa sitaki kuzungumza na
waandishi, mambo yangu yote wapo watu ambao wanaweza kuyazungumzia.”
Hata hivyo, katika hotuba yake, Rais Kikwete aliagiza kuchukuliwa hatua kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakimu Maswi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma kuhusu ushiriki wake kwenye kashfa
hiyo.
Chapisha Maoni