0
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo imepokea malalamiko kutoka kwa wasambazaji wa filamu kuhusu ushushwaji wa bei za filamu uliotangazwa na Kampuni
ya Steps Entertainment.

Wizara imeyashughulikia malalamiko hayo na kuona kuwa bei iliyotangazwa na Kampuni ya Steps Entertainment si halisi na itasababisha tasnia ya filamu
kudharauliwa na pia haina tija katika
tasnia ya filamu.

Wizara inaiagiza kampuni ya Steps
Entertainment kusitisha kuanza kuuza
filamu hizo kwa bei ya Tshs. 1000 mpaka
hapo muafaka utakapopatikana katika
kikao kitakachofaninya kati ya Wizara ya
Habari, Vijana,Utamaduni na Michezo,
Wizara ya Fedha na Wizara ya Viwanda na Biashara.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA
MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA
HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO.

Chapisha Maoni

 
Top