MKURUGENZI wa Benchmark Production, Rita Paulsen, ametolea ufafanuzi kuhusiana na mchakato wa kusaka waimbaji chipukizi katika
shindano lake maarufu la ‘Bongo Star Search’
linalofanyika kila mwaka.
Rita Paulsen
Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Rita
kutambulisha kipindi chake kipya cha televisheni
cha ‘Rita Paulsen Show’ kinachorushwa kila
Jumapili katika runinga ya Azam two.
“Rita Paulsen Show ni kitu ambacho kimekuwa
katika mawazo yangu zaidi ya miaka saba
nyuma, kwa hiyo ni cha siku nyingi ni mipango
ambayo nilikuwa nayo na sasa imetimia na ni
moja tu ya mambo ambayo yapo pamoja na
Bongo Star Search,” alisema.
Rita aliongeza kuwa, Bongo Star Search iko
palepale na kuwatoa hofu Watanzania, huku
akisema mazungumzo baina yake na uongozi wa
Azam Tv yanaendelea kuona uwezekano wa
kurusha matangazo ya kipindi hicho.
Kipindi cha Rita Paulsen Show ni kipindi cha
kijamii chenye vipengele vya kuelimisha na
kuburudisha familia.
Chapisha Maoni