May 4 2016 serikali kupitia wizara ya
Habari,Sanaa,Utamaduni na Michezo waliufungia
wimbo wa Chura pamoja na kumfungia msanii
Snura kimuziki kisha May 5 msanii huyo akawa
amekamilisha vitu vyote kisha akafunguliwa
kimuziki,kazi ikawa kwenye kuuachia wimbo wa
Chura ambao aliambiwa aurudie,kitu unachotakiwa kufahamu kwa sasa,ni kwamba
Snura aliandika script ya video lakini pia ilikataliwa.
Snura
‘’Nilipeleka script a video mpya ta Churs bodi ya
filamu ilichukua muda kidogo kuipitia nilifuatilia
sana ndio nikapewa majibu baada ya wao kukaa
kikao na kupitia wakaniambia kuwa ile script
hwajaikubali nishuti kwasababu wanasema
maudhui yake yanataka kufanana na ile video ya
mwanzo nilishindwa kuelewa kwasababu kwa
uelewa wangu niliona nimeandika kitu tofauti
kwasababu video ya mwanzo ilikuwa imechezwa
kwenye maji na wanawake ndio walikuwa
wanacheza lakini video hiyo ambayo niliyokuwa
nimeiandika ilikuwa ni mimi mwenyewe ndio
nitakuwepo kwenye hiyo video halafu sichezi
natembea huku naimba halafu watu wananiona
mie natembea huku naimba na wao wananifuata
kwa nyuma huku wanacheza naenda napanda
daladala na wao wanapanda nikishuka na wao
wanashuka huku wakicheza’’ Alisema Snura.
cloudsfm
Chapisha Maoni