0
Tanzania ni miongoni mwa mataifa chache duniani
yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.
Na baada ya kugunduliwa kwa gesi asili mkoani
Mtwara na dhahabu sasa watafiti kutoka Uingereza
wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi
adimu zaidi ya Helium kwa mujibu wa BBC.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha
Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini
kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban
futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama
inavyofahamika.
Ugunduzi huo umefanyika katika eneo la bonde la
ufa la Tanzania.
Katika taarifa kwa wanahabari huko Japan, watafiti
hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote
duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa
madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu
kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama
MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo
ya kinyuklia miongoni mwa sekta zingine nyingi za
kawi na teknolojia.
Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri
ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa
2035.
Mnamo mwaka wa 2010 Mwanfizikia mshindi wa
tuzo la Nobel Robert Richardson alikuwa ametabiri
kumalizika kabisa kwa gesi hiyo.
Ukosefu huo ulikuwa umesababisha wataalamu
kuhimiza kutungwa kwa sheria itakayopunguza
matumizi yake katika bidhaa zisizo za dharura
kama vile kwenye vibofu kutokana na hali ya kuwa
gesi hiyo ya Helium ni nyepesi kuliko ile ya
Oxygen.
"Gesi tuliyoipata nchini Tanzania inaweza kujaza
silinda za gesi milioni moja nukta mbili za
mashine za MRI" alisema Chris Ballentine kutoka
chuo kikuu cha Oxford.

Chapisha Maoni

 
Top