0
Mamia ya wanafunzi nchini MISRI wameandamana
mbele ya ofisi ya wizara ya elimu ya nchi hiyo
mjini CAIRO wakipinga kufutwa kwa mitihani ya
vyuo vya elimu ya juu.
Maandamano hayo yamefanyika baada ya maafisa
kumi na wawili wa wizara ya elimu ya nchi hiyo
kukamatwa kufuatia majibu ya masomo ya kiarabu,
dini na masomo mengine kusambazwa kwenye
mtandao wa Facebook mapema mwezi huu.
Majibu hayo yamesambazwa na mtu mmoja
asiyefahamika anayetumia mtandao huo kwa
madai ya kutaka kudhihirisha kuwepo kwa vitendo
vya rushwa pamoja na uzembe katika wizara
Mfumo wa Elimu wa MISRI umekuwa ukigubikwa
na msongamano wa wanafunzi kwenye vyumba
vya madarasa, walimu wenye kiwango kidogo cha
elimu hali inayowafanya mamilioni ya wanafunzi
ambao wazao wao wana uwezo kufundishwa
wahadhiri binafsi.

Chapisha Maoni

 
Top