Maendeleo(CHADEMA) Tundu Lissu ambaye pia ni
Mnadhimu Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
ameseme kuwa, vitendo vinavyofanywa na serikali
ya awamu ya tano ni vya hovyo.
Lissu ameyasema hayo muda mfupi baada ya
kumaliza kusikiliza shauri lake katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Kwenye shitaka hilo, Lissu pamoja na washitakiwa
wengine watatu wanadaiwa kufanya makosa
mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchochezi kupitia
gazeti la Mawio la tarehe 14 Januari 2016.
Kwenye gazeti hilo lililoandikwa kichwa cha habari
‘Machafuko yaja Zanzibar’ Lissu alinukuliwa kama
mchangiaji wa gazeti hilo ambapo tayari limefutwa
na serikali.
Nje ya mahakamani hiyo Lissu amesema “nchi
yetu imeingia katika giza nene, mambo
yanayofanywa na Serikali hayakubaliki.
“Kila msema kweli wa nchi hii, huu ni wakati wa
kujitokeza na kusema hii ni nchi ya vyama vingi,
hii ni nchi inayotambua haki za binadamu kwenye
Katiba yake.
“Hatuwezi tukakubali nchi iongozwe kwa kauli za
mdomo za mtu mmoja hata kama amechaguliwa
kuwa rais.”
Akizungumzia kesi iliyofunguliwa na kuhusishwa
kwake Lissu amesema, kesi iliyofunguliwa na
serikali dhidi yake na wahariri wa gazeti la Mawio
ya uchochezi, ni ushahidi tosha kuwa nchi
imeingia kwenye giza nene la udekikteta.
Amesema, hata sheria ya magazeti ya mwaka
1976 ipo wazi kwamba, kuikosoa serikali sio
uchochezi.
“Mashtaka haya yanayodaiwa kuwa ni ya
uchochezo, sio ya uchochezi hata kidogo.
Nilichosema, niliulizwa na waandishi … nilisema
uchaguzi wa marudio Zanzibar unaweza kuviingiza
visiwani hivyo kwenye machafuko na umwagaji
damu… ni kauli ya raia anayefahamu na
hapendezwi na mwenendo wa serikali” amesema
Lissu.
Amesema kuwa, hata sheria ya magazeti inasema
kuwa kitendo chochote chenye lengo la kueleza
ubovu wa serikali au mamlaka yake sio kosa.
“Nilichosema mimi kuwa serikali hii na matendo
yake ni ya hovyo… hali hii inahitaji kupingwa na
kila mwananchi,” amesema.
“Kama wanafikiria watatutisha kwa kutuleta
mahakamani, tutamkabili mahakamani na
tutamkabili nje.
“Ni wakati wa wazalendo kusema kuwa, Tanzania
ni nchi ya vyama vingi na ina Katiba na sheria.
"Katiba yetu inatambua haki za binaadamu na
moja haki za binaadamu ni kueleza ujinga wa
watawala wanapofanya ujinga,” amesema.
Mwanahalisi Online
Chapisha Maoni