0
Liverpool wamekamilisha usajili wa Sadio Mane
kwa pauni milioni 34 kutoka Southampton. Kitita
hicho kinamfanya kuwa mchezaji aghali zaidi
kutoka Afrika. Mane, 24, kutoka Senegal
amepachika mabao 21 katika mechi 67 za Ligi Kuu
ya England akiichezea Southampton tangu
alipohamia mwaka 2014 akitokea Salzburg. "Leo ni
siku kubwa, na nina furaha kusaini katika moja ya
timu kubwa Ulaya," Mane ameiambia tovuti ya
Liverpool.
"Ni klabu ambayo imeshinda vikombe vingi na ina
historia kubwa."

Chapisha Maoni

 
Top