moja mjadala wa vikao vya Bunge kama
ilivyokuwa awali, bado inaumiza wananchi
Safari hii wananchi wametinga mahakamani na
kwamba leo wamefika katika Mahakama Kuu
Kanda ya Dar es Salaam kufungua kesi ya
kuitaka mahakama hiyo kutengua agizo la
serikali la kuzuia matangazo ya moja kwa
moja ya Bunge.
Januari mwaka huu, Nape Nnauye, Waziri wa
Habari, Vijana, Utamaduni, Michezo na Sanaa
alilieleza Bunge hatua ya kuzuia matangazo ya
moja kwa moja ya chombo hicho kama
ilivyokuwa awali.
Miongoni mwa sababu alizotoa ni kwamba,
serikali imekuwa ikibeba mzigo mkubwa wa
gharama katika kuendesha matangazo hayo
pia watumishi wa umma kutumia muda
mwingi kuangalia Bunge badala ya kufanya
kazi.
Hatua ya serikali kuzuia kurusha matangazo
hayo ya moja kwa moja imeibua mjadala
mkubwa kitaifa ambapo kada mbalimbali
nchini zimekuwa zikipinga hatua hiyo.
Katika kesi iliyofunguliwa leo, ina walalamikaji
10 ambao ni Azizi Himbuka, Perfect
Mwasililwa, Rose Moshi, Penina Nkiya, Andrew
Mandari, Hilda Sigara, Juma Uloleulole, Kubra
Manzi, Ray Kimbito na Ben-Rabiu Saanane.
Kesi hiyo imesikilizwa na Profesa Ferdinand
Wambari, Jaji Kiongozi katika mahakama hiyo,
na jaji mwengine katika kesi hiyo Sakieti
Kihiyo, hata hivyo hakuwepo mahakamani leo.
Washtakiwa kwenye kesi hiyo ni Nape pamoja
na George Masaju, Mwanasheria Mkuu wa
Serikali (AG) ambapo Abubakari Mrisho, ndio
wakili wa upande wa walalamikiwa.
Kwa upande wa walalamikaji unasimamiwa na
Peter Kibatala na Omari Msemo ambao ni
mawakili wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema).
Kesi ya msingi iliyofunguliwa ni kuitaka
mahakama kutengua uamuzi uliotolewa na
Nape ambaye aliwasilisha kauli ya serikali
bungeni.
Walalamikaji wanaitaka mahakama itangaze
kuwa, Raia wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania wana haki ya kikatiba ya kujua
majadiliano yanayoendelea bungeni kwa
mujibu wa ibara ya 18(B), (d) na 29 (1).
Pili walalamikaji wamedai kuwa, serikali
imekiuka haki ya kikatiba kwa kuzuia bila
kuwa na sababu za msingi haki ya wananchi
kusikia majadiliano ya Bunge kwa kuzuia
kurusha matangazo ya moja kwa moja.
Tatu, walalamikaji wameitaka mahakama
kuilekeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kurejesha haki ya kikatiba ya
wananchi kwa kurusha matangazo ya moja
kwa moja ya Bunge.
Nne, walalamikaji wamedai kuwa, matokeo ya
kuzuia matangazo hayo ni kunyimwa kwa haki
za Watanzania kutokana na kushindwa
kuwasimamia pia kuwafuatilia wabunge na
mwenendo wao bungeni.
Tano, walalamikaji hao wamedai kuwa, sababu
za kuzuia matangazo hayo hazijitoshelezi
hivyo Watanzania na walalamikaji wanayo haki
ya kupata taarifa ya vikao vya Bunge kwa
maslahi ya taifa.
Hata hivyo upande wa utetezi ulidai kuwa,
walichelewa kupata taarifa ya mashtaka hayo
hivyo hawakupata muda wa kutosha wa
kuaandaa majibu. Kutokana na hivyo,
mahakama iliuambia upande wa walalamikiwa
kwamba, watajibu mashtaka hayo 15 Julai siku
ambayo kesi hiyo itatajwa.
Chapisha Maoni