zilizokuwa zinatoroshwa ikiwa ni siku kadhaa
baada ya Mkuu wa mkoa wa Tabora, Agrey Mwanri,
kutoa wiki moja kwa ajili ya wanaomiliki silaha
mkoani humo kuzisalimisha kwa hiyari.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Tabora, Kamishna Msaidizi wa
Polisi Khamis Selemani Issa, amesema silaha hizo
zilikuwa zinatoroshwa kutoka wilaya ya Kaliua
kwenda maeneo mengine baada ya amri ya mkuu
wa mkoa.
Kamanda Issa amesema kuwa kati ya
waliokamatwa ni pamoja na mtoto wa miaka 16
hiyo jeshi la polisi linachunguza kwa kina juu ya
umri halisi ya mtuhumiwa huyo aweze kufunguliwa
mashtaka kutokana na umri wake.
Kamanda huyo wa Mkoa wa Tabora ameendelea
kuwasihi wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha
sheria Mkoani humo kuendelea kuzisalimisha kwa
hiari na kusisitiza endapo mtu atakutwa katika
opresheni ya kuzisaka silaha hizo hatua kali
zitachukuliwa dhidi yake.
Chapisha Maoni