Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusiano na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na
Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
alipokutana na kufanya mazungumzo na
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli
akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya
kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi
Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.
Rais Azali Assouman pia amepongeza
jitihada zinazofanywa na serikali ya
awamu ya Tano zinazolenga kuhakikisha
wananchi wa Tanzania wanapata huduma
bora za kijamii na kusisitiza kuwa serikali
yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania
ili kutatua changamoto mbalimbali
zinazowakabili wananchi wa Komoro.
Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI
kwa Rais wa Comoro Azali assouman,
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan
amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa
Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati
ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za
elimu, afya na biashara kwa ajili ya
manufaa ya nchi hizo MBILI.
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa
Comoro kheri katika safari yake ya Mecca–
Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia
Suluhu Hassan amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa
nchini Masaharu Yoshida na kumweleza
kuwa serikali itaendelea kuweka na
kuboresha mazingira bora kwa ajili ya
wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali
Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka nchini
JAPAN.
Makamu wa Rais amesema serikali ya
JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa
maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili
miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania
Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu,
afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri
na lakuigwa na washirika wengine wa
maendeleo.
Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa
nchini MASAHARU YOSHINDA
amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA
SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea
kufadhili ipasavyo miradi ya maendeleo
hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa
Tanzania wanapata huduma bora za
kijamii.
Chapisha Maoni