bao 1-0 na TP Mazembe ya
DRC katika mchezo wa Kundi
A, Kombe la Shirikisho Afrika
jioni ya leo Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Hicho kinakuwa kipigo cha
pili mfululizo kwa Yanga,
baada ya Juni 19 kufungwa
pia 1-0 na wenyeji MO Bejaia
1-0 nchini Algeria.
Shujaa wa Mazembe leo
alikuwa ni Mereveille Boppe
aliyemalizia mpira wa adhabu
uliopigwa na beki Chrtistian
Luyindama dakika ya 74.
Katika mchezo huo ambao
mashabiki waliingia bure,
Mazembe walionyesha
kiwango kikubwa zaidi ya
Yanga kuashiria kwamba
walistahili ushin di huo.
Pamoja na ubora wa
Mazembe, lakini leo Yanga
ilicheza chini ya kiwango,
wachezaji wake wakionekana
kabisa kucheza kwa woga na
kutojiamini.
Shambulizi la maana la
Yanga lilikuja dakika ya 44 tu
baada ya mshambuliaji
Mzimbabwe kufanikiwa
kumzidi mbio na maarifa
beki Luyindama na kumpasia
kiungo Deus Kaseke
aliyepiga nje akiwa amebaki
na kipa, Sylvain Gbohouo
Guelassiognon.
Kipindi cha pili, Mazembe
walifunguka zaidi na
kupeleka mashambulizi
mengi langoni mwa Yanga
hadi kupata bao lao pekee.
Kiungo Mzambia, Obrey
Chirwa hakuwa na madhara
leo, wakati kiungo chipukizi
mzalendo Juma Mahadhi
alijitahidi ingawa hakuweza
kumaliza mechi baada ya
kuumia na kumpisha
Geoffrey Mwashiuya dakika
ya 69.
Kuelekea mchezo huo, Yanga
ilitumia muda mrefu
kulumbana na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) juu ya
matangazo ya Televisheni
hadi wakaamua kufuta
viingilio siku mbili kabla ya
mechi.
Yanga itahitimisha mechi
zake za mzunguko wa
kwanza za Kundi A kwa
kucheza na Medeama ya
Ghana Agosti 7 Uwanja wa
Taifa pia.
Vikosi kamili vya leo ni
Yanga; Deo Munishi ‘Dida’,
Juma Abdul, Mbuyu Twite,
Vincent Bossou, Kevin
Yondan, Thabani Kamusoko,
Haruna Niyonzima, Deus
Kaseke, Juma Mahadhi/
Geoffrey Mwashiuya dk69,
Obrey Chirwa/Matheo Simon
dk71 na Donald Ngoma.
TP Mazembe; Sylvain
Gbohoud Guelassiognon,
Jean Kasusula, Issama
Mpeko, Salif Coulibaly,
Rodger Asale, Adama Traore/
Deogratius Kanda dk76,
Merveille Bope, Nathan
Sinkala, Koffi Christian/Jose
Bodibake dk80, Christian
Luyindama na Thomas
Ulimwengu.
Chapisha Maoni