0
MPIRA UMEKWISHAAAAA
-SUB, Mazembe wanamuingiza Badibake
-KADI Assale analambwa kadi ya
njanoDAKIKA 4+ ZA NYONGEZA
KADI Dk 89 Ulimwengu analambwa kadi ya
njano
Dk 85 na 86, TP Mazembe wanaonekana
kuupoza mchezo taratibu kama
wameridhika na bao moja. Lakini Yanga
wawe makini na mashambulizi ya
kushitukiza
Dk 84, Ulimwengu anawatoka Twite na
Bossou na kupuga kupiga shuti, Yanga
washukuru unatoka juu kidogo. Ilikuwa
hatari sana
Dk 82, Kamusoko anapiga faulo safi kabisa
hapa...goal kick
Dk 80, Niyonzima anaangushwa nje ya
eneo la hatari, mwamuzi anasema faulo. Si
mbali sana na lango la Mazembe
SUB Dk 78 Mazembe wanamtoa Adama
Traore na nafasi yake inachukuliwa na Deo
Kanda
Dk 76, Ulimwengu anaingia vizuri hapa
anapiga shuti linakuwa butu
GOOOOOOOOOO Dk 73, Bope
anaukwamisha mpira wavuni baada ya
kujichanganya kuokoa baada ya mpira wa
faulo
KADI Dk 72 Yondani analambwa kadi ya
njano
Dk 72, Yondani anamuweka Ulimwengu
chini hapa, inakuwa ni ni, faulo nje kudogo
ya eneo la hatari
SUB Dk 71 Yanga wanamtoa Chirwa
anaingia Simon Matheo
Dk 70, Assale tena, anaingia vizuri na
kupiga shuti kali kabisa hapa
SUB Dk 69 Yanga wanamtoa Mahadhi
aliyeumia na nafasi yake inachukuliwa na
Mwashiuya
Dk 69, Ulimwengu anajaribu hapa shuti,
goal kick
Dk 68, Ulimwengu anamtoka hapa Yondani
lakini Kamusoko anawahi na kuokoa
KADI Dk 66, Twite anakuwa mchezaji wa
kwanza kulambwa kadi ya njano
Dk 60 na 61, mashambulizi ya zamu kwa
kila mlango, lakini hakuna shambulizi kali
kwa kuwa mabeki wanaokoa kwa urahisi
kabisa
Dk 59, kona inachongwa, Yanga
wanachelewa kuokoa lakini Nekandio
anashindwa kulenga lango na kuwa goal
kick
Dk 58, pasi nzuri ya Mahadhi lakini Asale
anatoa na kuwa kona, inachongwa,
Koulibaly anaokoa
Dk 55, Kasusula anamuangusha Mahadhi
hapa, mwamuzi anasema faulo, anaichonga
faulo Niyonzima, lakini laini kabisa
Dk 53, Asalle akiwa nje ya 18 ya Yanga
anaachia shuti kali lakini anashindwa
kulenga lango
Dk 51 hadi 52, Yanga wanamiliki mpira kwa
dakika mbili zote, hata hivyo mipango ya
umaliziaji inaonekana bado
Dk 50, MAzembe wanapata kona,
inachongwa na Asale, hatari hapa lakini
Twite anaokoa
Dk 47, Mazembe wanaonekana kuanza
kufanya mashambulizi na Yanga
wanapaswa kuwa makini na mipira ya juu
Dk 45 Kipindi cha pili Yanga wanaonekana
kuanza kwa kasi kabisa hapa. Ngoma
anakwenda chini baada ya kuumizwa
MAPUMZIKO
-Nafasi nyingine bora kabisa, Yanga
wanapoteza, Kaseke na Ngoma
wanashindwa kuwa na mawasiliano ndani
ya 18 ya Mazembe hapa
DAKIKA 1+ YA NYONGEZA
Dk 45, Asale anachonga kona nyanya
kabisa hapa, inakuwa goal kick
Dk 44 KAsusula anaichonga vizuri, Dida
anawahi kuanguka lakini anaugusa na kuwa
kona, inachongwa Twite anaokoa, kona tena
Dk 43, Asale alikuwa anakwenda hapa lakini
Mahadhi anamwangu na kuwa faulo
Dk 42 Ulimwengu anaingia vizuri akiwa
amebanwa na Yondani lakini anafanikiwa
kupiga shuti, si kali sana
Dk 39 hadi 41, bado hakuna ubunifu sana
kwa kipa upande na muda huu wote mpira
umechezwa katikati
Dk 37 na 38, TP wanaonekana kuupoza
mpira huku wakijipanga kwa pasi za
taratibu. Lakini mabeki wanafanya kosa
hapa na kipa anatoka na kuokoa
Dk 36, Twite anapiga shuti kali la mpira wa
adhabu...goal kick
KADI 35 Mpeko analambwa kadi ya njano
kwa kumuangusha Chirwa
Dk Dk 34, krosi nzuri ya Juma Abdul,
Ngoma anaukosa mpira akiwa hatua tatu
kutoka langoni. Hii ni nafasi nzuri zaidi
ambayo Yanga wamepoteza
Dk 30, Kaseke anaingia vizuri, kona.
Inachongwa vizuri na Niyonzima lakini
Mazembe wanaokoa hapa
Dk 28, Kamusoko anafanya kazi ya ziada
kuondoa mpira miguuni mwa Traore,
agauke na mpira na kuondosha
KADI Dk 27, Adama Traore wa MAzembe
analambwa kadi ya njano kwa
kumuangusha Juma Abdul
Dk 23 hadi 24, Yanga ndiyo wanaonekana
kuucheza sana mpira, lakini bado hawana
mipango ya umaliziaji
Dk 22 Chirwa anawatoka mabeki wa TP,
kwake Ngoma, anapiga krosi safi, Mahadhi
hatari hapa. Mpira anauwahi Niyonzima
unarudi na kukumuta Juma Abdul, anapiga
shuti linaokolewa, anapiga tena TP
wanaokoa hapa
Dk 20, Traore anaingia tena kwenye lango
anaingia na kupiga krosi safi, Dida anaokoa
na Bossou anatoa na kuwa kona...
Dk 15, Niyonzima anaingiza krosi safi
kabisa lakini kipa anatoka na kuokoa.
...faulo
Dk 12, Yondani anashika, mwamuzi
anasema faulo kwenda Yanga, anapiga
Kasusula, hovyoooo kabisa
Dk 11, hatari hapa, Chirwa anaingia lakini
Mazembe wanaokoa, Mahadhi anaingia
tena, kona. Inachongwa lakini haina
matunda
Dk 9, Juma Mahadhi anaingia vizuri kabisa
lakini MAzembe wanatoa na kuwa kona.
Inachongwa, Bossou hatariiiii lakini inakuwa
goal kick
Dk 7, Kipa Guela anafanya kazi ya ziada
kuokoa mpira wa faulo wa Kamusoko na
kuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, goal
kick..
Dk 5, Traore anaingia kwa kumtoka Juma
abdul, anapiga krosi safi kabisa, kona.
Inachongwa na Asale, off side
Dk 4, Mazembe wanagongeana vizuri na
kuingia kwenye hatari la Yanga, mpira
unatoka na kuwa goal kick lakini wachezaji
wa TP wanalalamika kuwa ni kona
Dk 3, Yanga wanakuwa wa kwanza kujaribu,
Juma Abdul anapiga shuti kali la mpira wa
adhabu....juuu
Dk 2, hakuna timu iliyofanikiwa kugusa
kwenye lango la mwenzake hadi dakika 2
na nusu za mchezo

Chapisha Maoni

 
Top