Bayern Munich Arjen Robben atakosa
kuanza kuitumikia timu yake katika
msimu mpya wa Ligi Kuu ya Ujerumani
Bundesliga kwa wiki 6 baada ya kuumia
nyama za paja.
Kinara huyo mwenye umri wa miaka 32
pia alikosa ligi ya msimu uliopita miezi
miwili ya mwisho baada ya kuumia.
Aliumia wakati timu yake ya Bayern
inajiandaa kucheza na Borussia
Dortmund katika mchezo wa mechi ya
ufunguzi wa ligi, Ujerumani Super Cup
Agosti 14 mwaka huu. Ligi ya Ujerumani
inatarajia kuanza kutimua vumbi hapo
Agosti 26 mwaka huu ambapo Bayern
Munich itafungua dimba na Werder
Bremen.
Chapisha Maoni