0
Klabu ya soka ya Hull City imethibitisha
kuwa kocha wake Steve Bruce
amefanyiwa usaili na chama cha soka
cha Uingereza ili aweze kuwa kocha
mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo.
Uongozi wa timu hiyo umesema kuwa
Steve Bruce amefanya mazungumzo na
wakuu wa FA ila hakuna taarifa yoyote
rasmi iliyotolewa na FA kuhusu suala
hilo. Timu hiyo iliyorejea ligi kuu msimu
huu imesema inataka suala hilo
limalizike mapema ili kuweza kuepuka
uvumi pamoja na kumpa nafasi kocha
wao kuianda timu yao kwa ajili ya
msimu mpya wa ligi kuu ya Uingereza.
Kocha wa Hull City
Martin Glenn ambaye ni Mtendaji Mkuu
wa FA ataongoza jopo la watu watatu
ambao ni mkurugenzi wa ufundi wa FA,
Dan Ashworth pamoja na mjumbe wa
bodi chama hicho, David Gill ili kuamua
nani anastahili kupewa jukumu hilo la
kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya
Uingereza.
Akiwemo Steve Bruce tayari FA
wameshamfanyia usahili kocha wa
Sunderland, Sam Allarddyce au Big Sam
huku kocha wa timu ya Bournemouth,
Eddie Howe na kocha wa timu ya taifa ya
Marekani, Jurgen Klinsmann nao
wamekuwa wakihusishwa kupewa kazi
hiyo!

Chapisha Maoni

 
Top