0
“Guardiola kwa sasa ni kati ya makocha
bora na hakuna na shaka kwa hilo. Ana
elimu kubwa tangu aanze kufundisha
soka, katika kipindi kilichopita tulikuwa
tukichukua makocha kutoka ugenini.
Lakini kwa sasa makocha wetu ndio
wanakwenda kufundisha nje, tunajivunia
kuwa na makocha kama Guardiola.
Hatukuweza kuwa na makocha kama
huyu katika kipindi cha nyuma,” alisema
kocha Vicente del Bosque ambaye ni
mkufunzi wa zamani wa timu ya taifa ya
Hispania amemtaja Pep Guardiola kuwa
ndiye atakayekuwa mkufunzi wa timu
hiyo na huku akisema kuwa suala la
kuzaliwa Catalan halitakuwa tatizo kwa
kocha huyo mpya wa Man City.
Kocha Del Bosque alijiengua kwenye
kikosi cha Hispania baada ya kikosi
chake kutupwa nje ya michuano ya
fainali za Euro 2016 wakiwa hatua ya 16
bora, lakini akiwa ameshaiwezesha timu
hiyo kutwaa ubingwa wa dunia mwaka
2010 na wa michuano hiyo ya Euro
2012. Tangu kocha huyo aondoke,
Guardiola ni miongoni mwa makocha
wanaotajwa kuwania nafasi hiyo, licha ya
kuwa ndio kwanza ametua Man City na
Del Bosque anaunga mkono kocha huyo
kukiongoza kikosi hicho.

Chapisha Maoni

 
Top