0

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF), limetangaza
rasmi ratiba ya Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara
msimu wa mwaka 2016/2017, huku ikizipanga
timu za Simba na Yanga kukutana Oktoba mosi
katika mchezo wa mzunguko wa kwanza
utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TFF
kupitia kwa Ofisa Habari wake, Alfred Lucas,
michuano hiyo itaanza rasmi Agosti 20, ambapo
mechi saba zitachezwa kwenye viwanja tofauti
ukitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya
Yanga na Azam utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam, Agosti 17.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa ratiba imezingatia
michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa
ngazi ya klabu na timu za Taifa, ili kukwepa dhana
yoyote ya upangaji wa matokeo na kurundikana
kwa michezo.
“Hii ni ratiba rasmi ukiachana na ile ambayo
ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, tunaomba
familia ya soka kuegemea kwenye hii ya sasa
rasmi inayotolewa na TFF.
“Ile ya mitandao ya kijamii imekosewa anuani ya
Posta ya TFF, kadhalika kuonesha kuwa mchezo
kati ya Azam FC na African Lyon ungefanyika
Agosti 21, 2016 ilihali hii rasmi ina anuani sahihi
na mchezo huo wa raundi ya kwanza ukionesha
utachezwa Agosti 20, 2016,” alisema.
Hata hivyo, katika ratiba hiyo Yanga itacheza na
Azam Oktoba 16 ikiwa ugenini, wakati Simba wao
watakutana na Azam Septemba 17.



Posted Africa News Sports

Chapisha Maoni

 
Top