Meya wa Manispaa ya Ubongo Jijini Dar es Salaam, Boniface Jacob Leo amefungua Mtaa ambao umepewa jina la Kiungo wa Kimataifa kutoka nchini Kenya na Timu ya Tottenham Hotspur ya England Victor Wanyama.
Akifungua Mtaa huo Meya Huyo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, amesema kwamba amefurahishwa na kazi nzuri anayoifanya Wanyama kutangaza vyema soka la Afrika Mashariki na Ndio Maana wameamua kumzawadia mtaa huo.
Awali Mtaa huo ulikuwa ukifahamika kwa jina la Viwanjani na hivyo kwa mantiki hiyo sasa Utaitwa Victor Wanyama Street.
Wanyama ambaye yupo mapumzikoni Jijini Dar es Salaam toka Mwanzoni mwa Juma, ameonekana kuridhishwa na mapokezi mazuri aliyoyapata iwemo kuhudhuria michuano ya Ndondo Cup iliyokuwa inaendelea katika uwanja wa Kinesi uliopo Ubungo.
Chapisha Maoni