0
Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu amewatoa hofu mashabiki wa Mshambualiaji Mrundi Laudit Mavugo kuwa hatoondolewa katika kikosi hicho msimu ujao.
Kaburu amesema japokuwa kumekuwapo na minong'ono Ya chini kwa chini juu ya kumuacha Mrundi huyo Lakini hakupata maagizo yoyote kutoka kwa Kocha Joseph Omog hivyo wanyaiga wazi kuwa bado Yupo katika mipango yake msimu ujao.
-Laudit Mavugo Bado ni mchezaji muhimu kwenye timu na hataachwa niwahakikishie hivyo, Bado ana mkataba na Mwalimu anamuhitaji na tunaongeza watu kwenye eneo lake ili kuongeza changamoto kwa kuwa msimu ujao tuna mashindano mengi ambayo yanahitaji tuwe na kikosi kipana Zaidi,”Kaburu Alieleza.
Hofu ya wapenzi wa Mavugo inakuja wakati Simba wakiwa katika Usajili kabambe ikiwemo kuwasajili wachezaji wazuri katika eneo la ushambuliaji kama Mzambia Walter Bwalya, Mganda Emanuel Okwi na Donald Ngoma kutokea Yanga.
Ikumbukwe kuwa Mavugo alijunga na Simba msimu uliopita akitokea kwa Mabingwa wa ligi ya Burundi Vital’O na amefanikiwa kufunga mabao saba katika Ligi na kuiwezesha Simba kumaliza nafasi ya pili.

Chapisha Maoni

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top