Ufaransa baada ya kuichapa Wales mabao 2-0
katika mchezo mkali na wa kusisimua.
Tangu awali Ureno ilikuwa inapewa nafasi kubwa
ya kuibuka na ushindi katika mpambano huo wa
nusu fainali licha ya kuwa haijafanya vizuri sana
katika michezo yake ya awali.
Luis Nani na Cristiano Ronaldo ndio walioiwezesha
Ureno kuibuka na ushindi muhimu unayoiwezesha
timu hiyo kutinga hatua ya fainali kwa mara ya
kwanza nje ya dimba lao la nyumbani.
Wales ilicheza vyema kipindi cha kwanza hata
hivyo mabao ya haraka haraka ya Ureno
yaliyofungwa ndani ya dakika tisa za mwanzo
kipindi cha pili yalifuta ndoto ya Wales kutinga
fainali yake ya kwanza katika michuano ya Ulaya.
Ureno sasa inamsubiri mshindi wa mchezo
mwingine wa nusu fainali kati ya wenyeji Ufaransa
dhidi ya Ujerumani utakaopigwa Alhamisi, Julai 07,
saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.
Chapisha Maoni