Kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ambaye alitangaza kuachana na soka, amezidi kuishangaza familia ya wapenda Soka nchini baada ya kusema yupo tayari kuifundisha Timu yoyote ile ikiwemo Timu ya Soka ya Yanga.
Julio ambaye ni mnazi wa muda mrefu wa Timu ya Simba amesema kutokana na ubora wake katika kulifundisha soka yupo tayari kuifundisha Timu yoyote ile, ila Timu hiyo iwe tayari kuweka mezani kiasi kikubwa cha Pesa ili kuweza kumshawishi kurejea tena Katika kulifundisha soka.
-Yoyote anayetaka Mimi nikaifundishe Timu yake Aweke kwanza Mzigo mezani mimi nitakwenda, hata Yanga akiweka Pesa za Maana nitaenda kuifuindisha, watanzania watasema nimefunza kanuni za usimba na Uyanga lakini hapo ndipo wanapofeli, Toka dunia imeubwa adhana haijawahi kubadilika” Julio Alieleza.
Alivyojiuzulu.
Mwishoni mwa mwaka jana Julio alitangaza kustaafu soka akiwa na Timu ya Mwadui FC kwa kile alichodai kuwa Maamuzi mabovu ya waamuzi wa soka nchini na toka kipindi hicho hakuwahi kujihusisha na timu yoyote ile licha ya kutajwa pengine angeirithi nafasi ya ukatibu mkuu wa klabu ya Simba baada ya Kuondoka kwa Patrick Kahemele.
Chapisha Maoni