0
WAKATI wananchi wakiwa bado hawajarizika kuhusu Hatua alizochukua Rais Jakaya Kikwete, Juu ya maamuzi ya Bunge kuhusu ufisadi wa Zaidi bilioni 306 kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow, kutokana na Rais Kikwete kulikejeli Bunge kwa kuyatupia mbali
mapendekezo mengi ya Bunge.

Nao Umoja wa Vyama vya vikuu vya Upinzani nchini ambavyo vinaunda Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA vimeibuka na kumvaa Rais Jakaya Kikwete na kusema anahusika kwa kiasi kikubwa kwenye Ufisadi
huo, kwa kitendo chake cha kumtetea Mmiliki wa wa kampuni ya Independent power limited (IPTL), Bwana Harbnder Singh (Singasinga).

Na Kusema Umoja huo utaanzisha
Maandamano nchi nzima kupinga Ufisadi huo ambao wanadai unalindwa na Rais Kikwete kutokana na yeye kuhusika katika Wizi huo.

Kauli hiyo ya Vyama hivyo vikuu vya Upinzani vinavyounda UKAWA umetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha
Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba wakati wa mkutano na waandishi wa Habari uliohitishwa Mahususi ili kuzungumzia hutuba
ya Rais Kikwete kuhusu sakata hilo ambapo Profesa Lipumba alisema inasikitisha kuona Rais Jakaya Kikwete ameacha kulitetea shirika la Umeme Tanesco na kuwatetea Matapeli wa
IPTL ambao wameliingizia hasara la mabilioni ya Fedha shirika hilo.

“Hotuba ya Rais kikwete imekuwa mtetezi mkubwa wa Mmiliki wa PAP,anaacha kulitetea shirika la umma la Tanesco,harafu anadanganya umma kwa kiasi kikubwa kusema kwamba pesa za IPTL si za Umma hivi anashindwa hata kuelewa Ripoti ya
Mkaguzi Mkuu wa Serikal CAG ambayo
inaonyesha wazi kwamba wamiliki hawa
wamefanya utaperi wa wazi kabisa katika umiliki wake “ “Taarifa za mauzo ya Kampuni ya Mechmar kwenda piper link kwenda PAP ziliwasilishwa
katika taasisi mbalimbali za Serikali na bwana Singh sote tunafahamu ni kughushi nyaraka ili akwepe Kodi na hili ni kosa, hivi Kikwete alioni hili?”alihoJi Profesa lipumba.

Profesa lipumba alizidi kusema hata Maazimio yanayotokana na Taarifa ya CAG yanaonyesha wazi kuwa PAP siyo mmiliki wa halali wa hisa za Kampuni ya Mechmar lakini Rais Kikwete
hakuliona hilo.

Kwa Upande wake Katibu mkuu wa Muungano vyama hivyo wa Vya Upinzani vinavyounda
UKAWA ambaye pia naye ni Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dokta Wilbroad Slaa amesema Umoja umepanga kuzunguka nchi nzima ikiwemo kuandaa maandamano kupinga kile wanachodai Rais Jakaya Kikwete amewalinda
wezi wa Ufisadi huo.

Dokta Slaa aliongeza kuwa Kitendo cha Rais kikwete kuwatetea Wamiliki wa kampuni ya IPTL ni wazi Rais Kikwete anahusiki kutokana na kuwepo kwa ushahidi wa yeye kuhusika na
Wezi huo.

“Tunajua wazi kwamba Rais kikwete kuhusika na wizi huu kwani kuna mtu mmoja anaitwa Guruma ambaye katika watu waliopewa pesa na bwana James Rugemalira jina lake limetajwa kupokea mabilioni ya Fedha na mtu huyo mimi namfahamu sana, Bwana Guruma
anajulikana sana ni msimamizi wa Miradi ya Rais kikwete na leo kachukua pesa za Escrow unategemea nini hapa na ndio maana anasuasua kuwachukulia hatua wamiliki wa IPTL”Alisema Dokta Slaa.

Aidha,Dokta Slaa alisema kitendo cha Ufisadi huo kutokea na Idara ya Usalama wa Taifa kushindwa kulinda nchi kwenye ufisadi huo ni wazi idara hiyo imeshindwa kazi.

“Usalama wa Taifa upo kila Balozi inashangaza sana kuona Idara hii inashindwa kuona utapeli wa mmiliki wa IPTL au tutegemee nini ndio
maana hata kwenye Ufisadi wa EPA,tuliona Jinsi Kampuni iliyokuwa ikimilikiwa na Ofisa wa Usalama wa Taifa ilivyochota pesa unategemea nini”

“Na hata Kikwete alivyosema mara baada ya kutua uwanja wa ndege alipotoka kutibiwa anavyosema alijui sakata hili kutokana na yeye kuwa kwenye matibabu , ni kuwadanganya
watanzania kwani baada ya masaa mawili kutoa uwanja wa ndege hapo,niliona email aliyekuwa akitumiana na bwana Rugemalira, sasa huyo ni kiongozi kweli”alihoji Dokta Slaa.

Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR
Mageuzi James Mbatia alisema ni Rais kikwete amekosa maamuzi katika nchi kutokana na kitendo chake cha kushindwa kuwachukulia hatua waliohusika na kusema pesa za
wananchi zimepotea huku taifa likikosa fedha hususani wao wabunge mpaka sasa hivi hakuna hata mbunge aliyepata hata mshahara.


Umoja huo wa UKAWA ni muunganiko wa Vyama vya CHADEMA,CUF na NCCR pamoja NLD

Chapisha Maoni

 
Top