0
 SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo na
Elimu ya Juu Nchini wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kwa kutoa maamzi kwa wale ambao walihusika katika sakata la akaunti ya Tegeta Escrow na kwa kutengua uteuzi wake kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi , Profesa Anna Tibaijuka, kujiuzulu kwa aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema pamoja na kusimamishwa kazi kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliackim Maswi.

Akizungumza na waandishi wa habari
katika ofisi ndogo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ,jijini Dar es Salaam, Mtendaji wa Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo na Elimu ya Juu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Christopher Ngubiagai, alisema maamuzi magumu ya Rais Jakaya Kikwete ni jambo
la busara kwani Watanzania walikuwa
wakisubiri kwa hamu maamuzi yake katika sakata la Tegeta Escrow.

Ngubiagai alisema nchi inajengwa na
viongozi walio bora kuchukua maamzi pale ambapo linatokea jambo, kuweza kuchukua hatua kwa wale ambao wamekwenda tofauti ambayo ndio demokrasia imara kwa wananchi.

Aidha alisema katika hotuba ya Rais Jakaya Kikwete alipokutana na Wazee wa Jiji la Dar es Salaam Desemba 18, mwaka huu a kuwa hakuna sababu ya kutaifisha mali za muwekezaji kutokana na mfumo uliopo sasa ni ushirikiano wa Sekta Binafsi (PPP).

Wananfunzi hao waliwataka Watanzania
kuwa na imani na Rais Kikwete kutokana
na utendaji wake unaoonekana katika
maamzi mbalimbali ili kuhakikisha
wananchi wanapata maendeleo na kuweza kuondokana na umasikini ambayo ndio ilani ya CCM.
Katibu Mtendaji Mkuu wa Shirikisho la
Vyuo vya Elimu nchini wa Chama cha
Mapindizi (CCM), Ndugu Christopher
Ngubiagai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) juu ya maamzi aliyochukua Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sakata la Tegeta Escrow. Wengine ni Katibu wa Mkoa Dar es Salaam wa Shrikisho hilo David Zenda (Kulia), Mwenyekiti wa UWT Chuo Kikuu Huria Tawi la Ilala Evelyne Chack (kushoto).

>> Africa Newss

Chapisha Maoni

 
Top