Dar es Salaam. Serengeti Boys imeanza vizuri mashindano ya kusaka kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika ‘Afcon’ baada ya kuichapa Burundi kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo.
Katika mchezo huo mabao ya Serengeti Boys yalifungwa na Kelvin John dakika 11 na Agiri Ngoda dakika 28, huku bao la kufutia machozi la Burundi lilifungwa na Nibikora Arthar.
Serengeti Boys ilianza mchezo huo kwa kasi, lakini washambuliaji wake walikosa umakini katika kumalizia nafasi nyingi walizopata.
Tanzania ilipata bao la kuongoza dakika ya 11, lililofungwa na chipukizi Kelvin akimalizia vizuri pasi ya Alphonce Msanga hata hivyo shangwe za mashabiki wa Serengeti Boys zilidumu kwa dakika 9 tu kabla ya Burundi kusawazisha dakika 20 kupitia Nibikora aliyetumia vizuri makosa ya mabeki wa Tanzania kufunga goli hilo.
Dakika ya 28, Ngoda alifanya kile kilichosubiliwa na mashabiki wa Tanzania baada ya kupachika bao la ushindi akimalizia pasi safi kutoka kwa Kelvin John.
Dk 34 Kelvin John alishindwa kutumia nafasi ya wazi aliyoipata akiwa yeye na kipa Burundi baada ya shuti lake kupaa juu ya goli.
Tanzania iliendeleza mashambulizi langoni mwa wapinzani wao na kufanikiwa kupata kona dakika ya 36 ambayo haikuzaa matunda kutokana na mpira kutoka nje kidogo ya lango.
Ushindi huo unaifanya Tanzania ipande hadi nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa sawa na Rwanda kwa pointi, lakini wakitofautiana mabao ya kushinda. Rwanda katika mchezo wake wa kwanza ilishinda 3-1 dhidi ya Sudan.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.