Kikosi cha Simba imeshindwa kutamba mbele ya Namungo FC kwa kwenda suluhu ya 0-0 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Ruangwa, Lindi.
Katika mchezo huo uliopigwa ndani ya Uwanja wa Majaliwa Simba walionekana kupata nafasi nyingi zaidi na kuonesha asilimia kubwa ya umiliki wa mpira japo nyavu zikashindikana kutikishwa.
Mech hiyo imepigwa Ruangwa ikiwa ni maalum kwa ajili ya kuuzindua Uwanja huo wa Majaliwa ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.
Baada ya mchezo huo, Simba wataendelea na mazoezi baada baada ya kesho kujiwinda na Mtibwa Sugar kuelekea mechi ya Ngao ya Hisani.
Simba watakuwa wanakipiga na Mtibwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Agosti 18 baada ya kuutwaa ubingwa wa VPL 2017/18 huku Mtibwa wakichukua Kombe la Shirikisho.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.