MABAO ya N'Golo Kante dakika ya 34, Jorginho kwa penalti dakika ya 45 na Pedro dakika ya 80 yameipa Chelsea ushindi wa 3-0 dhidi ya Huddersfield katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa John Smith leo.
Katika michezo mingine iliyochezwa leo Fulham ikiwa nyumbali ilikubali kipigo cha mabao 0-2 kutoka Crystal Palace shukrani kwa magoli ya Schlupp, Zaha.
Bournemouth ilitumia vizuri uwanja wake wa nyumbani kuichapa Cardiff mabao 2-0 yaliyofungwa na Fraser na Wilson). Mabao mawili ya Pereyra yalitosha kuipa Watford ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton, wakati mapema Tottenham ilishinda 2-1 dhidi ya Newcastle.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.