England. Mabao yaliyofungwa na beki wa Tottenham, Jan Vertonghen na Dele Alli yalitosha kuwanyamazisha Newcastle United katika mechi ya kwanza ya Ligi Kuu msimu huu wa 2018/19.
Mchezo uliopigwa muda mfupi uliopita kwenye uwanja wa James' Park na wenyeji kuondoka vichwa chini wakishindwa kuamini matokeo hayo.
Tottenham, timu iliyoandika historia kwa kuwa ya kwanza kutosajili mchezaji katika dirisha la kiangazi tangu kuasisiwa kwa mfumo wa usajili wa kiangazi mwaka 2003, iliutawala mchezo kwa kiasi kikubwa.
Timu hiyo ndiyo iliyoanza kujipatia bao la kuongoza likifungwa na Vertonghen aliyemalizia mpira wa kona uliochongwa na Cristian Eriksen na kuguswa na Davinson Sanchez kabla ya kumkuta mfungaji aliyepiga kichwa cha nguvu.
Wenyeji walitulia na kusawazisha bao hilo dakika tatu baadaye baada ya Joselu kupiga kichwa cha kuchupia krosi ya Matt Ritchie, akimuacha kipa Hugo Lloris hana la kufanya.
Hata hivyo mshambuliaji kinda wa Uingereza, Dele Alli hakufanya ajizi zaidi ya kuipa Spurs bao la pili katika dakika ya 18 mabao yaliyodumu hadi mwisho wa mchezo na kuiwezesha Spurs kuanza Ligi vema.
Newcastle ilipoteza nafasi mbili za kusawazisha katika dakika ya pili ya kipindi cha pili, Mohamed Diame alipiga shuti lililogonga mwamba na dakika nne baadaye Kenedy naye akapoteza nafasi nzuri aliyoipata.
Matokeo benchi Salomon Rondon, aliyenunuliwa siku ya mwisho ya dirisha la usajili akitokea West Bromwich Albion, alikaribia kuifungia Newcastle zikiwa zimesalia dakika tano baada ya shuti lake kumbabatiza Vertonghen na kugonga mwamba.
Mfungaji bora wa fainali za Kombe la Dunia 2018, Harry Kane, aliendelea kukosa mabao katika mwezi Agosti akifikiza mechi 14 za Ligi bila kufunga ndani ya mwezi Agosgti licha ya misimu mitatu mfululizo kuibuka mfungaji bora wa Tottenham.
Chapisha Maoni
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.