0
NYOTA wa Barcelona, Neymar amefunga mabao mawili katika ushindi wa 4-0 wa timu yake ya taifa, Brazil dhidi ya Uturuki usiku wa kuamkia leo Uwanja wa Sukru Saracoglu.

Neymar aliwafungia bao la kwanza mabingwa hao mara tano wa Kombe la Dunia dakika ya 20, kabla ya beki wa Uturuki, Semih Kaya kujifunga kuipatia Brazil bao la pili dakika ya
24.

Willian akawafungia Brazil bao la tatu dakika ya 44, kabla ya Nahodha Neymar kuhitimisha ‘pati la mabao’ kwa kuifunga bao la nne timu ya Carlos Dunga dakika ya 60.

Kikosi cha Uturuki kilikuwa; Demirel, Kaya, Koybasi, Irtegun, Tufan, Kisa, Altintop, Turan, Topal, Bulut na Erdinc.


Brazil: Diego Alves, Danilo, Miranda, Luiz, Luis, Fernandinho, Oscar, Gustavo, Willian, Luiz Adriano na Neymar.

Chapisha Maoni

 
Top