
Washindi hao wa pili wa Kombe la Dunia Julai mwaka huu, walilazimika kutoka nyuma ili kupata ushindi huo, baada ya Anas Sharbini kuifungia Croatia bao la kuongoza dakika ya
11.
Argentina ilipata bao la kusawazisha kupitia kwa Cristian Ansaldi dakika ya 48, kabla ya Lionel Messi kufunga la ushindi kwa penalti dakika ya 57 kufuatia Sergio Aguero kuangushwa kwenye eneo la hatari.
Mshambuliaji Carlos Tevez alipata mapokezi mazuri aliporejea Upton Park baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Aguero.
Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero,
Zabaleta, Vergini, Fazio, Ansaldi/Silva dk76, Perez, Mascherano, Banega/Pereyra dk70, Di Maria/Lamela dk76, Messi na Aguero/Tevez
dk61.
Croatia: Lovre Kalinic/Vargic dk88, Vrsaljko, Leskovic/Mitrovic dk83, Jedvaj, Badelj, Leovac, Milic/Tomecak dk70, Kovacic/Halilovic dk46, Antolic, Sharbini/Jajalo dk64 na Cop/Rog dk83.
Chapisha Maoni