
kuuawa.
Mauaji hayo yalitokea juzi na jana kwenye vijiji vya Kazinguru na Lamrambogo katika Kata ya Matui ambako watu zaidi ya kumi na mmoja
wanadaiwa kujeruhiwa huku maboma 14 ya wafugaji yakichomwa moto na wakulima na mifugo kadhaa kuuawa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo waliokuwa kwenye Zahanati ya Matui jana wakisubiri miili ya marehemu na majeruhi wa vurugu hizo, walidai
chanzo cha mauaji hayo ni kifo cha mkulima mmoja aliyeshambuliwa na wafugaji.
Mmoja kati ya mashuhuda hao, Mbwana Juma alisema mkulima huyo alikuta mifugo imeingia shambani kwake na kula mihogo, na alipouliza jambo hilo, wafugaji wakamkatakata na kumuua.
Alisema baada ya wakulima kupata taarifa ya kuuawa kwa mwenzao, ndipo walipochukua silaha za jadi na kuwaua wafugaji wawili, mwanamke na
mwanaume na kukamata mifugo ambayo waliichinja na kula nyama.
Alisema baada ya wafugaji kuona wenzao wameuawa kwa mapanga na sime, ndipo baadhi yao walipochukua silaha za baridi na za moto ikiwamo bunduki na kuwaua wakulima wanne.
Kuna hofu kuwa maiti zaidi zzipo eneo hilo.
Alisema hadi jana jioni, hali ilikuwa tete eneo la Matui na maduka yalikuwa yamefungwa huku shughuli zote zikiwa zimesimama kwa hofu ya
vurugu.
Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Manyara, SACP Deusdedit Nsimeki, akizungumza kwa njia ya simu jana jioni, alithibitisha kuuawa kwa watu
watano kwenye eneo hilo la Matui.
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Martha Umbullabalisema kwa njia ya simu wakati akielekea eneo la tukio kuwa hajapewa taarifa ya idadi kamili ya
watu waliouawa.
Chapisha Maoni