
Agizo hilo lilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Simbachawene alipokuwa akijibu swali
kwa niaba ya Waziri Mkuu. Alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Meatu,
Meshack Opulukwa (Chadema) ambaye alitaka kujua kama ni halali kwa sungusungu kuamrisha, kuwacharaza bakora viongozi wa dini hata kama
viongozi hao wana makosa.
Simbachawene alisema serikali inatambua na kuheshimu kazi nzuri inayofanywa na sungusungu katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Hata
hivyo, alisema sungusungu wanahitaji kufanya kazi yao kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo pamoja na kuheshimu haki na uhuru wa
wananchi kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Alisema tayari serikali ilishaomba radhi kwa viongozi wa dini na inaendelea kuomba radhi, kwa si uungwana kufanya vitendo vilivyofanywa na watu.
Alisema adhabu ya viboko bado inatumika katika maeneo mbalimbali nchini na kwamba haijafutwa,
isipokuwa hutolewa kwa utaratibu maalumu baada ya kupata vibali.
Chapisha Maoni